Shughuli za kibiashara zilisitishwa kwa muda katika eneo la suswa kufuatia maandamano ya wenyeji wa eneo la suswa kutoka jamii ya wamasai . Wenyeji hao zaidi ya mia tano wanalalamikia kunyakuliwa kwa ardhi ya umma katika eneo hilo. Wakati huohuo wenyeji wa elgeyo marakwet wametaka kuondoka mara moja kwa kampuni za kigeni za mbao kufuatia tetesi kuwa zimepewa kipao mbele kukata miti kwenye msitu ulio katika eneo hilo.