Chama cha ODM kimebadilisha katiba yake kuwaruhusu wanachama wowote kuwania kiti cha urais. Mwafaka huu ulifikiwa katika mkutano wa baraza kuu la chama hicho. Hapo awali katiba ilimruhusu kiongozi wa chama Raila Odinga kuwa mgombeaji wa kipekee na kupelekea aliyekuwa makamu wake musalia mudavadi kukihama chama hicho. Kiongozi wa chama raila odinga na mwenyekiti henry kosgey walitangaza kuwa hawataungana kumziba yeyote asikipate kiti cha urais.