Mdahalo uliokuwepo kuhusu sketi za wanafunzi wa kike huenda umefikia kikomo hii leo baada ya wizara ya elimu kuonyesha sampuli za sketi wanazopaswa kupewa wasichana. Waziri Mutula Kilonzo amenukuu kifungu cha sheria kinachohitaji kuhusishwa kikamilifu kwa wanafunzi, kuhusu maamuzi yanayowagusa moja kwa moja.