Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya shule na wahusika wake wanao waacha wanafunzi kuendelea na masomo wakati wa likizo ,haya ni kwa mujibu wa Waziri wa Elimu Mutula Kilonzo.Waziri Mutula alidokeza kuwa ni jukumu la shule na walimu kujikakamua kuhakikisha kuwa wanakamilisha mtaala wa elimu kwa wakati ufaao bila kuingilia likizo ya wanafunzi.