Julius Yego jana alasiri alivunja rekodi yake ya kitaifa katika mchezo wa kurusha tufe ya mita 79 nukta 95 baada ya kurusha tufe kwa umbali wa mita 81 nukta 12 kwenye makala ya mwisho ya Finnish Elite Games mjini Kuortane. Yego ndiye mwakilishi wa kenya wa pekee katika michezo ya uwanja.