Madereva, Makondakta na wakazi wa eneo la Mazeras Mombasa mapema leo wamefanya maombi ya kipekee kufukuza mapepo ya ajali ambayo wanadai yamekuwa yakisababisha ajali kila uchao katika eneo la Bonje na kuua watu. Kwa kipindi cha majuma mawili yaliyopita zaidi ya ajali tatu zimetokea eneo lilo hilo na takriban watu 20 wamekufa. tunampisha John Juma na ripoti ya kina.