Huku hayo yakijiri eneo la nyando , naye miguna miguna anaaminika kuondoka kutoka humu nchini hapo jana usiku mwendo wa saa tano , miguna anaaminika kubebwa na ndege ya kampuni ya klm iliyokuwa ikielekea amsterdam uholanzi , na kupitia mtandao unaodaiwa kuwa wake mchana kutwa miguna amezungumzia sababu yake kuondoka humu nchini pia kudhihirisha stakabathi anazodai ni za mikakati iliyoandaliwa kwenye mikutano ya kampeini za chama cha odm mwaka wa 2007 anne ngugi na maelezo hayo