Shirikisho la soka nchini, FKF limekata kauli kwamba kocha mpya wa timu ya taifa, Harambee Stars atatoka nje ya kenya. Jambo hilo limepingwa vikali na wakufunzi wa humu nchini huku wakisema ni matayarisho duni yanayochangia kudorora kwa timu ya taifa na wala si wakufunzi. Sasa msema kweli ni nani?