Mtoto anapozaliwa kila mama huwa na haja ya kumuona mwanawe akiwa katika hali njema baada ya kujifungua na pia akiwa katika hali bora. Lakini hii haikuwa mtazamo wa mama Naomi anayefahamaika kama lucia ngendo kariuki alipojifungua mwanawe wa kike na wa mwisho. Kwani wakati aliponyeshwa baada ya yeye kutiwa katika chumba cha watoto wachanga, ni kana kwamba kitovu cha kichanga kilikuwa kimetoka nje na mala ya tumbo ya mwanawe wa kike. Na hapo alikanaa kwamba huyo sio mwanawe wa kweli. Lakini kwa miaka saba hadi sasa alikubali hali hio ya kiafya iliyomkumba mwanawe na nia yake anataka tuu mwanawe aishi maisha ya kama ya kawaida bila ya vitisho au kuchokozwa na wenzake wakati wanapocheza wenzake wakubali hali yake kwani sio mapenzi yake bali ni jinsia ya kimwili inayohitaji tuu ni matibabu.