Waziri mkuu Raila Odinga ametaka wamiliki wa shirika la shelter afrique kuondoa kinga za kidiplomasia dhidi ya mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, alasan ba, ili aweze kushitakiwa chini ya sheria za Kenya. Karen Kandie ambaye ni mfanyakazi wa shirika hilo anadai kudhulumiwa na alasan. raila ameonya kuwa iwapo shirika hilo halitaondoa kinga za kidiplomasia, ataagiza waziri wa mambo ya nje pamoja na mkuu wa sheria kumfurusha raia huyo wa kigeni.