Sekta ya utalii inasalia juu kwenye orodha ya zile zinazoinua uchumi wa kenya. Na japo wengi wanafahamu vyema wanyama wanaojumuishwa kwenye sekta hii,wachache wanajua kuhusu ngombe spesheli wanaojulikana kama ankole. Ngombe hawa wana pembe ndefu mno kiasi cha kuwashangaza wengi iwapo hao ni ngombe. Ni wanyama kutoka nchi jirani ya uganda wanaohifadhiwa katika hifadhi moja huko laikipia. Ankole waliletwa kutoka uganda katika mwaka wa 2004 kwasababu wamo katika hatari ya kuangamia kwa kiingereza . Carol Nderi alizuru hifadhi ya ol pejeta laikipia na kutuandalia taarifa ifuatayo.