Wakaazi wa kaunti ya Nyandarua wametishia kufika mahakamani kusimamisha kubomolewa kwa nyumba zaidi ya mia moja zilizojengwa wakati wa ukoloni . Wakaazi hao wanasema kuwa kuna njama ya watu binafsi kunyakuwa ardhi baada ya nyumba hizo kubomolewa . Wakaazi hao aidha wametaka nyumba hizo za kihistoria kuhifadhiwa ili kuwa kivutio cha kitalii.