Huku Ulimwengu ukiadhimisha siku ya Kimataifa ya idadi ya watu, ni wazi kwamba watu wanaongezeka sawia na idadi ya vifo inayoendelea kuongezeka. Kina mama wajawazito ndio wanaoathirika pakubwa,jambo lililopelekea kampuni ya Phillips kutekeleza mojawapo ya malengo ya millennia kwa kutoa vifaa vya kuangalia kizazi haswa kwa waja wazito kwa kimombo ultra scan machine. Hata hivyo wakazi wa kijiji kimoja huko Uasin Gishu wameelezea hofu zao dhidi ya kifaa hicho ambacho ni kigeni mbele ya macho yao na badala yake kusema kuwa wameridhika na huduma za wakunga.