Ibada ya Wafu ilifanywa huko Mwingi kwa watu kumi waliofariki kufuatia mashambulizi yaliyotekelezwa katika makanisa mawili tofauti huko Garissa wiki moja iliyopita. Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka aliwaongoza wenyeji wa eneo hilo katika kutoa heshima za mwisho kwa waumini hao wa kanisa la AIC ambao walikutana na mauti yao wakiwa kanisani. Kwenye ibada hiyo idara ya polisi ililaumiwa vikali , kwa kile kinachotajwa kuwa uzembe wa kuhakikisha usalama umedumishwa kote Nchini. Frank Otieno alihudhuriashughuli hiyo na sasa anatupasha zaidi.