Mara nyingi idadi kuu ya watumishi wa Mungu wakiwemo makasisi na mapadre hutimiza majukumu yao ya kueneza injili bila ya kugusia masuala ya ziada. Lakini katika eneo la Kieni kaunti ya Nyeri, padre mmoja wa Kikatoliki anafahamika mno kama mwanzilishi wa miradi mbalimbali inayowanufaisha wakaazi wa Mlima Kenya. Ni raia wa Italy lakini ameishi Kenya tangu mwaka wa 1971 na kutangamana na wakaazi kiasi cha kufahamu lugha wanayoizungumza. Sio mwingine bali ni Father Romano Filipe kutoka nchi ya Italy na anayefahamika zaidi na wenyeji kama mzungu anayezungumza Kikuyu kwa ufasaha. Mwanahabari wetu Carol Nderi alikutana na Father Romano na amemhoji katika makala ya leo ya darubini.