Mahakama ya Mombasa imemwachilia huru jamaa aliyeshukiwa kutekeleza shambulizi la kigaidi eneo la Mshomoroni wiki mbili zilizopita na kusababisha vifo vya watu watatu. Mahakama hiyo imesema polisi hawakuweza kutoa ushahidi wa kutosha katika kuthibitisha kuwa jamaa huyo alihusika. Wakti huo huo viongozi wa dini na madhehebu yote mjini Mombasa pamoja na viongozi wa vyombo vya usalama eneo hilo wamekubali kushirikiana ili kuondoa hofu ya uwezekano wa kuchipuka kwa uhasama wa kidini kutokana na mashambulizi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakilenga makanisa.