Dereva wa gari la aina ya mitsubishi evo 9, Alistair Cavenagh leo anasherehekea ushindi wake katika mbio za magari ya KCB s & l mortgage loan zilizo kamilika katika eneo la Kwale, Mombasa. Cavenagh ambaye alikuwa ameshindwa mkondo wa kwanza hapo jana alijikakamua na kushinda mbele ya Peter Horsey na Ian Duncan.