Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha USIU ameripotiwa kuuawa na wenzake baada ya kutekwa nyara wiki iliyopita. Sarah Aruwa alitoweka anakoishi huko Roysambu, katika barabara ya Thika Jumamosi wiki iliyopita, na kisha watekaji wake kumpigia mamake simu wakidai malipo ya shilingi laki moja, lasivyo wamuue.