Serikali imeelekeza maafisa mia saba wa usalama katika mkoa wa kaskazini na kuwahamisha wakuu wa mikoa katika juhudi za kuimarisha usalama kwenye mipaka ya kenya na humu nchini. Kaimu waziri wa usalama wa nchi yusuf hajji alisema hatua hiyo itaepusha taifa na maafa. Aidha rais mwai kibaki amesema kenya haitotishwa na magaidi katika juhudi za kurejesha amani mpakani mwa kenya na somalia. Wakati huohuo makamu wa rais kalono musyoka na waziri mkuu raila odinga wameshinikiza wananchi kusaidia maafisa wa usalama kuimarisha uchunguzi.