Mashirika yanayojihusisha na michezo nchini yatapunguziwa matoleo yao ya ushuru pindi tu mswada wa michezo utakapopita bungeni. Waziri msaidi wa michezo Kabando wa Kabando alisema haya wakati ambapo kampuni ya DSTV ilikabidhi vyombo vya kupeperusha matangazo ya michezo hiyo halikadhalika kufuata matangazo hayo kupitia kwa Supersport bure bilashi kwa muda wa mwezi mmoja.