Wanawake waja wazito huhitaji mapenzi na kutunzwa na walio karibu nao kama vile kupelekwa kliniki na kuangaliwa hali yao ya kiafya. wanaume katika jamii hata hivyo wamekosolewa kwa kutochukua majukumu hayo wakae wake wao wanapokuwa waja wazito. tulipiga darubini katika kliniki za humu nchini kuangalia ni wanaume wangapi wanaojuhusisha katika afya ya wake zao wanapokuwa waja wazito . ikilinganishwa na wanaume katika mataifa kama tanzania ambapo wengi wao wamejitokeza kuwasimamia wake wao katika wakati huo mgumu .