Wakaazi wa kijiji cha kambirwa wilayani muranga’ mashariki walipigwa na butwaa wakati jamaa mmoja alipofanya majaribio ya kupaa kwa ndege katika uwanja mdogo wa ndege. Ijapokuwa ilimchukuwa Gabriel Nderitu miaka mitatu kuiunda ndege hiyo, haikupaa angani lakini anaimani kuwa ndoto yake itatimia siku moja.