Taharuki na huzuni imetanda mjiniMombasa kufuatia mlipuko uliotokea usiku na kusababisha vifo vya watu watatu na kuacha zaidi ya watu ishirini na majeraha mabaya. Wakazi wa mji huo hasa walioathiriwa wameghadhabika jinsi vyombo vya usalama vinatoa hakikisho kuwa usalama upo imara ilhali wanazidi kushambuliwa na jamaa zao kupoteza maisha. Mwanahabari wa KTN mjini Mombasa, John Juma anayo taarifa hiyo kwa ukamilifu.