Wakati ambapo kumeripotiwa visa vya uhasama kati ya wanyama pori na binadamu nchini, kule Naivasha katika mtaa wa lake view, kulitokea nyoka mkubwa aliyewatia hofu wakaazi wa mtaa huo. Ilibidi ujasisri wa Afisa mmoja wa vetinary kumuondoa nyoka huyo ambaye kisha alipelekwa katika mbuga ya wanyama ya Hells Gate.