Vuguvugu la Marafiki wa Raila, FORA, limepata mlezi mpya aliyejiunga katika harakati za kuhakikisha Waziri Mkuu Raila Odinga atashinda uchaguzi mkuu ujao. Mbunge wa Imenti ya Kati Gitobu imanyara, ambaye alitangazwa naibu mlezi wa FORA, alisema hatua hiyo ni mojawapo ya mikakati ya kuhakikisha Kenya inapata viongozi wenye misingi ya kubadilisha taswira ya siasa za Kenya. Aidha Waziri Mkuu Raila Odinga alisema wataunganisha viongozi zaidi waliohusika katika mageuzi ya demokrasia ya taifa hili katika kampeini yake. Sherehe hio iliandaliwa katika makao makuu ya FORA kama anavyoarifu Ali Manzu.