Biwi la simanzi lilitanda katika eneo bunge la Ndhiwa, wakati wa mazishi ya aliyekuwa waziri msaidizi katika wizara ya usalama wa kitaifa hayati Joshua Orwa Ojode. Marehemu Ojode ametajwa kama kiongozi mcheshi, mwenye bidii na aliyejitolea sana kwa kile alichokifanya. Rais Mwai Kibaki na viongozi wengine waliohutubu katika hafla hiyo waliwataka wakenya wote kudumishi amani kama njia mojawapo ya kutimiza safari ambayo wawili hao walikuwa wameainza.
Kibarua kilichoko kwa sasa ni kusaka viongozi watakaochukua nafasi ya ojode na aliyekuwa waziri wa usalama wa kitaifa marehemu profesa George Saitoti.