Kwa sasa itakuwa vigumu kidogo kwa wataalamu wa kuchunguza mkasa wa ajali ya ndege kutoka ufaransa kuendelea na uchunguzi rasmi hadi pale tume iliyoundwa itakapoidhinishwa baada ya kutangazwa rasmi katika gazeti la serikali. Kando na hayo kumekuwa na cheche za maneno kuhusiana na ajali ya ndege huku madai ya saitoti kuzimwa kisiasa yakipewa kipau mbele.