Kongamano la siku mbili kujadili mikakati ya amani kabla ya uchaguzi mkuu ujao limekamilika huku vyombo vya usalama nchini vikitoa tahadhari na maonyo makali kwa wanasiasa dhidi ya kutumia mbinu zinazoweza kulemaza amani kama vile kujenga uhusiano na makundi haramu na kutumia lugha ya uchochezi katika kampeni na mikutano ya kisiasa. Na hata waliohudhuria walipofumukana ujumbe mkuu waliotoka nao baada ya kukaririwa na kila mnenaji ni kuhakikisha amani ipo imara katika msimu wa uchaguzi.