Rais mstaafu Daniel Moi ameongeza kayuli yake, katika wito kwa wanasiasa kuwa wahubiri wa amani na kuendeleza kampeini zao bila semi za uchochezi. Moi akizungumza huko Nakuru alisema hasara iliopatikana kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi, ni funzo kubwa kwa wakenya, kuwa amani ndio ngao yao.