Sekta ya bima nchini inakabaliwa na changamoto za kibiashara kutokana na visa vya moto ambavyo vimeonekana kusababishia hasara kubwa. Katika mkutano wake wa kila mwaka kampuni ya bima ya kenya re imeelezea wasiwasiwake kutokana na madai ya malipo ya visa vya moto ambavyo viliripotiwa kwa wingi mwaka uliopita ikilinganishwa na miaka ya awali.