Je umaarufu wa Eugene Wamalwa umefifia tokea musalia mudavadi, ahame chama cha odm? Jana alionekana na kalonzo musyoka,na leo amesisitiza tena hatoungana na makundi yenye nia moja tu ya kumzuia waziri mkuu raila oldinga kuingia ikulu. New ford kenya iliomtongoza na kumtangaza wamalwa kuwa ni mgombea wake wa urais, sasa imempa kisogo. Madai pia yamejitokeza kuwa waziri huyo wa sheria ametuma risala kwa raila odinga iwapo atanyoosha mkono kumpokea katika basi la chungwa. Je eugene wamalwa kakosa makao?