Klabu ya AFC Leopards bado haijasajili mchezaji wa Tusker, Paul Were, kinyume na ripoti kuwa mshambulizi huyo ameshajiunga na timu ya Ingwe. Kocha mkuu wa AFC leopards Jan Koops amesema kwamba klabu yake bado inawania kusajili Were lakini Tusker inasema mchezaji Were hajaamua kama atasalia Ruaraka ama atakihama kwenda kwa Leopards.