Aliibuka mwanafunzi bora wa mtihani wa KCSE wa mwaka jana katika kaunti ya taveta lakini wasichokijua wengi ni kwamba kijana paul mwangura hakutarajia hata kumaliza masomo yake ya shule ya upili kutokana na tatizo la ukosefu wa karo. Na hata alipomaliza shule hakuwa na pa kwenda , na kuishia kupewa hifadhi na hoteli moja katika kaunti hiyo akitumai kwamba atapata uwezo wa kwenda chuo kikuu. Lakini juu ya yote haya bado hajakata tamaa ya kujiunga na chuo kikuu na kuendeleza ndoto yake ya kupata elimu maishani. Esther kahumbi na maelezo zaidi kumhusu.