Zaidi ya wakimbizi 1,500 wanaoishi kwenye kambi katika kaunti ya Nyandarua wameishtaki serikali kwa kushindwa kuwapa makao kama ilivyowaahidi baada ya ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007. Wakimbizi hao kutoka sehemu mbalimbali nchini tayari wamewasilisha kwa mkuu wa sheria na katibu katika wizara ya mipango maalum ilani ya kuipeleka serikali mahakamani.