Licha ya kutoshiriki katika mbio zake alizozoea za mita elfu tano na kumi, vivian cheruiyot hakuwa na bughudha zozote katika kumduwaza lucy kabuu kwenye mbio za mita 1500. Wanariadha wengi waliotamba katika mbio mbalimbali kutoka kikosi cha polisi hawakushiriki mashindano hayo yaliyofika tamati yake hii leo katika uga wa moi sports center kasarani.