Mamia ya wakimbizi kutoka nchini Sudan kusini wanazidi kuwasili katika kambi ya wakimbizi ya kakuma katika eneo la turkana. Wakimbizi hao wanaendelea kuingia nchini baada ya hofu ya kuzuka kwa vita baina ya taifa la sudan kusini na sudan kuhusiana na mzozo wa visima vya mafuta.