Rais mstaafu Daniel arap Moi ameonya wakenya dhidi ya kubebwa na wimbi la vyama vya kisiasa hasaa vinavyoundwa kwa msingi ya maeneo. Akizugumza katika makao yake huko kabarnet baada ya kufanya mazungumzo ya kipekee na waandishi habari wa KTN, Rais mstaafu aliwataka wakenya kutumia uhuru wao wa kidemokrasia kudadisi azma ya vyama na viongozi wao kabla kuviunga mkono. Aidha vikao vya hivi majuzi katika maeneo ya mkoa wa kati na Rift Valley chini ya miavuli ya Gema na Kamatusa vimetifua mjadala kuhusu siasa inayoendeshwa humu nchini wakati Kenya inapoelekea katika uchaguzi mkuu.