Wabunge wa ODM watimuliwa kwenye kamati

Na Mike Nyagwoka

Chama cha ODM sasa kina siku 14 kuwateua wawakilishi wake wapya wa kamati za bunge baada ya kuwaondoa wabunge waliokiasi chama hicho. Miongoni mwa walioondolewa ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Ababu Namwamba ambaye aliyekuwa katika Kamati za Bajeti, Kamati ya Usalama na ile ya Utekelezaji Katiba.
Mbunge wa Karachuonyo, James Rege ameondolewa katika Kamati ya Kawi na ile ya Utangamano wa Taifa huku mbunge wa Mathare, Stephen Kariuki akiondolewa katika Kamati ya Elimu na ile ya Utekelezaji Katiba. Wengine waliotimuliwa ni Mbunge wa Tigania Mashariki, Mpuri Aburi, Mbunge wa Imenti ya Kati Iringo Kubai, John Waluke wa Sirisia na Mbunge Maalum, Isaac Mwaura.
Baadhi ya wabunge hao wamelalamikia hatua hiyo wakisema inawanyima haki ya kuwahudumia wapigakura waliowachagua.

 

Related Topics

ODM Ababu Namwamba