Chama cha ANC ki tayari kujiunga na vyama vingine vya upinzani

Na Sophia Chinyezi
Chama cha Amani National Congress, ANC ki tayari kujiunga na vyama vingine vya upinzani ili kubuni muungano thabiti.
Kiongozi wa chama hicho, Musalia Mudavadi amesema wamekuwa wakishauriana na baadhi ya vyama kuhusu suala hilo, ili kuhakikisha upinzani unashinda uchaguzi ujao.
Kadhalika amesema wako tayari kuwapokea viongozi wengine ambao watavihama vyama vyao, wakiwamo wale ambao hawajaridhishwa na chama kipya cha Jubilee.
Ameyasema hayo Ijumaa mjini Machakos baada ya mkutano wa pamoja wa Kamati Kuu ya Kitaifa na kundi la wabunge.