Mikakati ya kukabili uuzaji dawa za kulevya yazinduliwa

Na,Sophia chinyezi
Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Dawa za Kulevya na Uhalifu, UNODC Jumatatu imezindua mpango ambao unalenga kuboresha mikakati ya kukabili uhalifu wa kupanga na ulanguzi wa dawa za kulevya. Mpango huo vilevile unatarajiwa kupiga vita ufisadi na ugaidi nchini na eneo zima la Afrika Mashariki.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Inspekta Mkuu wa Polisi, Joseph Boinett amesema utasaidia katika ukusanyaji wa taarifa za ujasusi na ushirikiano miongoni mwa idara za usalama.
Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Githu Muigai amesema miongoni mwa masuala ambayo yametambuliwa wakati wa uzinduzi ni kuyumba kwa masuala ya siasa na uchumi miongoni mwa mataifa ya eneo la Afrika Mashariki. Kadhalika amesema ni lazima utafiti wa kutambua vitisho na jinsi vinavyopangwa kufanywa ili kukabili changamoto kuhusu usalama.