Tobiko apata idhini kuendeleza mashtaka dhidi ya washukiwa wa ufujaji fedha za NYS

Washukiwa 11 wanaohusishwa na ufujaji wa shilingi milioni 791 kupitia miradi ya Taasisi ya Taifa ya Huduma za Vijana, NYS wamepata pigo mapema leo baada ya Mahakama Kuu kupinga ombi lao la kutaka kumzuia Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Keriako Tobiko kuwafungulia mashtaka ya ufujaji.
Miongoni mwa washukiwa hao ni mfanyabiashara Ben Gethi, mamaye Charity Wangui, Josephine Kabura na wakili Patrick Ogolla.
Watuhumiwa hao walimtaka Jaji Joseph Onguto kutoa agizo la kutofunguliwa mashtaka kwa misingi kwamba hakuna ushahidi wa kuthibitisha kwamba walihusika na ufujaji. Onguto hata hivyo amesema Tobiko hakukiuka sheria kwa kuagiza kuushtakiwa kwao.
Washukiwa wamekuwa kwa kipindi kirefu wakipinga kufunguliwa mashtaka suala lililosababisha kutoitikia mashtaka katika Mahakama ya Milimani.
Tobiko alipendekeza wathumiwa hao kumi na mmoja kufunguliwa mashtaka hayo ya ufujaji mnano mwezi Februari mwaka huu.

Na, Sulleiman Yeri

Related Topics