×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Mohamed Ali's Jicho Pevu: Mbona serikali iwape polisi magari ya vita?

County_Nairobi
 Armoured Personnel Carrier Photo:Courtesy

Hawakukosea waliposema: “Don’t be afraid to stand for what you believe in, even if you stand alone”. Ndo maana nauliza, je mwaona ninachoona? Kuna shida Kenya na ndio maana lazima tuambiane ukweli.

Sheria haipo tena — ole wako wewe unayesoma haya makala iwapo ulidhania kuna sheria. Mahakama zimejaa uozo, bunge ni bunge la maslahi na mamluki wa kizazi kipya, serikali za kaunti zimejaa wizi, polisi ndio majaji na mawakili, uongozi wa taifa umesalia uchi.

Hamna kinachosonga mbele na sasa macho yote yameelekezwa kwa uchaguzi mkuu ujao. Majuzi niliona vifaa vya kijeshi vya kivita vikikaguliwa rasmi na rais Uhuru Kenyatta katika. Uhuru alisema vifaa hivyo ni za kupambana na shida za usalama wa taifa.

Wengi waliamini lakini mimi nina wasiwasi. swali langi kwenyu wenye elimu ni, vifaa hivi vyafaa kuwa mikononi mwa wanajeshi au polisi? Sikatai GSU wana mafunzo kiasi ya kijeshi lakini iwe vipi leo wapewe wao badala ya wanajeshi wetu wanaopambana na Alshabab? Hebu tudadisi maswalihaya.

Jee, ni utaratibu gani uliofuatwa kati ya serikali ya Kenya na ile iliyotuuzia magari hayo ya kivita? Ni pesa ngapi zilizotumika kununua vifaa hivyo? Na je, wana GSU wana elimu na ujuzi wa kutumia magari hayo ya bomu?

Nauliza haya kwa sababu huenda magari haya yakawa ya mkopo, hivyo basi kuzidi kuwaangamiza wakenya na madeni. Huenda magari haya yakawa mabovu na kutumia jina la usalama wa taifa kuwahadaa wakenya. Ni sharti kama wakenya na walipa ushuru tuulize maswali haya kwa manufaa yetu sote. Ninahofia taifa hili ni la kuabudu wezi sugu na kuwatetea bila ya kujifikiria. Nahofia pesa za wakenya zinazidi kufujwa kila kukicha kwa misingi ya siasa chafu ndani ya idara za ki-usalama nchini. Nahofia kenya inazidi kubakwa na wahuni wakuu.Hofu langu kuu ni kuwa vifaa hivi si vya kutukinga na maadui bali ni vya kuafikisha malengo ya uchaguzi wa mwaka wa 2017 kwa mabavu.

Nahofia wakenya wakiinuka na kukataa maamuzi ya uchaguzi vifaa hivi huenda vitatumiwa dhidi ya wakenya.

Fungueni macho na mtazame nchi jirani ya Burundi.Sisemi tutachinjana bali nasema nina hofu ya jinsi viongozi wa Afrika hutumia mabavu kutawala. Kumbuka, maafisa fulani wa polisi waliwaua waandamanaji mwaka wa 2007 kama wanyama. Hadi wa leo hamna polisi aliyeshtakiwa.

Kila kukicha ila kila kukicha naomba Mungu atuvukishe katika chaguzi ijayo kwa njia salama salimin maana wanaotafuta nguvu kupitia damu za wakenya si haba na hawajali kwani lao kuu ni kutaka kuongoza kutoka kila kona ya taifa hii. Enyi wakenya, msiogope kuuliza maswali kwa sababu ni zamu ya makabila yenu kuiba na kubaka. Ulizeni kwa sababu ni zamu ya kutetea maisha ya watoto wenu. Serikali ya Jubilee imeonyesha tangu mwanzo kuwa haina nia njema kwa wakenya. Ufisadi, wizi wa mali ya umma, wizi wa ardhi, dhulma, ahadi tasa, hali mabaya ya usalama wa taifa na mambo mengine mengi yamekithiri.

Huenda labda naota ama nina mawazo mengi lakini ipo siku mtanikumbuka kwa semi hizi zangu. Ipo siku mtakubaliana na kauli hii yangu.

Tumewaona marais wa bara la Afrika wakifanya kongamano huko Ethiopia. Badala ya kujadili umoja wa afrika, biashara, ukulima na miundo misingi, walienda kujadili jinsi ambavyo watajiondoa kutoka mahakama ya jinai ya ICC ili kila wanapowafanyia unyama raia wao kote barani afrika, basi hawana wa kuwapigania wanyonge. Hawa ndio viongozi wenu wa kizazi kipya. Nilidhani watazungumzia Burundi na utawala wa mabavu lakini wapi! Jameni hamwoni ama mie ndiye kipofu? Mohammed

Ali ni Mhariri Mkuu wa Kitengo cha Upekuzi KTN. Kuwasiliana naye: [email protected], FB: Official Jicho Pevu with Mohammed Ali, Twitter: @mohajichopevu

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles